BURNA BOY AANDIKA HISTORIA MPYA UFARANSA
Burna Boy Aandika Historia Mpya Ufaransa!
Paris, Ufaransa — HISTORIA IMEANDIKWA!
Msanii maarufu wa Afrobeats kutoka Nigeria, Burna Boy, ameweka rekodi mpya kwa kuuza tiketi zote za tamasha kubwa ndani ya miezi michache tu, nje ya msimu wa matamasha (off-cycle), katika Uwanja wa Paris La Défense Arena — uwanja wenye uwezo wa kuchukua maelfu ya mashabiki.
Tamasha hilo la kihistoria limepewa jina la "No Sign of Weakness", na liliandaliwa kwa kiwango cha juu na kushuhudia maelfu ya mashabiki wakifurika kwa ajili ya burudani ya hali ya juu.
Burna Boy hakuonesha udhaifu hata kidogo! Aliwashukuru kwa dhati mashabiki wake na wasanii waliopanda jukwaani naye kwa kuandika:
“I’m so thankful for you all!! Big love to all my people that graced the stage with me! I appreciate every last one of you!”
Wasanii Waliosindikiza Tamasha Hilo
- Youssou N’Dour – gwiji wa muziki barani Afrika
- Santandave – msanii wa Hip Hop kutoka Uingereza
- Dadju, Joé Dwèt Filé, na We Re Noï – waliosababisha shamrashamra za kipekee
- Shallipopi – anayejulikana kama Waziri wa Furaha
- Fireboy DML, Nissi, Spaceship Billy, na DJ Lambo – waliofungua tamasha kwa kishindo
Kwa maneno ya Burna Boy mwenyewe, tamasha hilo lilikuwa ni:
“WHAT A TIME!?”
Ni wazi kuwa Burna Boy anaendelea kuandika historia kama mmoja wa wasanii wakubwa zaidi wa Afrika kwa sasa.
#JaylayTunes | #BurnaBoyLive | #AfrobeatsToTheWorld | #NoSignOfWeakness
PICHA: Kwa hisani ya @nickieleerose na



Comments
Post a Comment