PAPA FRANSIC AFARIKI DUNIA - HISTORIA YAKE MPAKA KIFO
JaylayTunes
Nyimbo Mpya Kila Siku!
Papa Francis Afariki Dunia – Historia Yake Mpaka Kifo
VATICAN CITY, Aprili 2025 – Katika tukio la kuhuzunisha, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ameripotiwa kufariki dunia leo saa 1:35 asubuhi akiwa katika makazi yake ya Kipapa huko Vatican. Kifo chake kimetokana na mshtuko wa moyo (stroke) uliosababisha kushindwa kwa moyo wake kufanya kazi, akiwa na umri wa miaka 88.
Papa Francis alizaliwa kama Jorge Mario Bergoglio mnamo Desemba 17, 1936, nchini Argentina. Alipata umaarufu kwa kuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini, na pia Papa wa kwanza kutoka Shirika la Yesu (Jesuits). Alijulikana kwa upole wake, kujali watu wa kawaida, na kupigania haki za kijamii, amani, na mazingira.
Alianza kazi yake ya upadre mwaka 1969, na kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires mwaka 1998. Mnamo Machi 13, 2013, alichaguliwa kuwa Papa wa 266, akichukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyejiuzulu.
Katika miaka yake zaidi ya 10 kama Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis alikumbukwa kwa hotuba zenye kugusa mioyo, uongozi wa huruma, na kuwafikia watu wa dini tofauti kwa njia ya maelewano. Salamu zake za mwisho za Pasaka zilikuwa “Hatujaumbiwa mauti bali uzima”.
Kwa sasa, dunia nzima inaomboleza na kuungana katika sala. Tunatoa pole kwa waumini wa Kanisa Katoliki duniani na kwa jamii nzima ya Wakristo.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, Na Mwanga wa Milele Umuangazie. Apumzike kwa Amani. Amina.



Comments
Post a Comment